Sunday , 1st Mar , 2015

Msanii wa muziki AT, ametoa ujumbe mzito kwa mashabiki wake na vijana kwa ujumla kufahamu umuhimu wa kujiandikisha kupiga kura, akiungana na kampeni ya ZamuYako2015 inayoendeshwa na kituo hiki.

AT

Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha vijana kushiriki katika masuala ya kisiasa hususani uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

AT ambaye amerejea katika chati na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina Sijazoea, amewataka vijana kutambua kuwa, nafasi ya kufanya maamuzi ya maendeleo yao ipo katika kupiga kura, na si kupuuzia na kulalamika pale wanapoona uongozi uliopo hauwatendei kama vile ambavyo wao wangependa.

Star huyo wa muziki amesema kuwa, ni vizuri kuwa sehemu ya uchaguzi wa uongozi uliopo, na si kuwa sehemu ya maandamano kupinga pale wanavyoviona si sawa katika uongozi.

Kijana #ZamuYako2015, Usichukulie Poa, Kajiandikishe.