
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David A. Misime amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wengine wa haki jinai linaendelea na uchunguzi wa tukio hili tangu taarifa hii ilipopokelewa ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Ameeleza kuwa Pamoja na ushahidi wa kisayansi ambao umeshakusanywa, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mwenye ushahidi wa ziada wa kusaidia kuthibitisha kilichomtokea binadamu mwenzetu hadi kupoteza maisha asisite kuuwasilisha ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ziweze kuchukuliwa.