Saturday , 11th Nov , 2023

Msanii wa BongoFleva Hussein Machozi ametoa ya moyoni kuhusu kuchukizwa na baadhi ya watu kumuita mzee wakati anadai yeye bado ni kijana mdogo na hata miaka 40 hajafikisha.

Picha ya Hussein Machozi

"Mimi nina akili sana, sijui kwanini watu wanataka kunifanya kama mkubwa sana nashindwa kuelewa. Wananiona mtu mzima kwa sababu ya hizi busara ama nini? Sipendi mnavyonizeesha wakati hata miaka 40 bado" amesema Hussein Machozi 

Msanii huyo kwa sasa anaishi nchini Italy akiwa na mke na watoto wake.