Wednesday , 8th Nov , 2023

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), kukagua viwanda 12 vinavyozalisha bidhaa za afya ili kuiwezesha MSD kununua kwa wazalishaji hao

Hatua hiyo inakuja kufuatia serikali kupitia Wizara ya Afya kuwapa meno Bohari ya Dawa (MSD), katika uzalishaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Alisema hali hiyo itaiwezesha Serikali kuokoa sh bilioni 300 iwapo viwanda vya ndani vitazalisha bidhaa za afya.
Naye Mkurugenzi wa Tehama kutoka (MSD), Leopord Shao, alisema maamuzi hayo ya serikali ni muhimu kwa kuwa bajeti ya MSD kununua bidhaa za afya ni sh bilioni 590 kwa mwaka, lakini asilimia 80 ya fedha hizo sawa na sh. bilioni 300 inatumika kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi, huku kiasi  kidogo ambacho ni sh. bilioni 100 ndiyo kinabaki ndani ya nchi.