Saturday , 4th Nov , 2023

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kimewataka wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo  kujitokeza kwa wingi kumlaki na kumpokea Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa 31 wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU)

Tulia amekuwa  mwanamke wa kwanza kutoka bara la Afrika kushika nafasi hiyo  katika uchaguzi uliofanyika Jiji la Luanda nchini Angola Oktoba  27,2023.

DK Tulia amechagulia kushika wadhifa  huo ulifanywa na baraza la 147 la (IPU) lilojumuhisha wabunge kutoka duniani  ambacho ndicho chombo kikuu kinachofanya maamuzi ambapo nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Duarte Pacheco kutoka Ureno ambaye ameitumikia nafsi hiyo kwa miaka mitatu.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 4 2023 katika Ofisi za Chama Mkoa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela amesema baada ya kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mbeya  kukutana na kujadili  mambo kadhaa kuwa kamati hiyo imepongeza Dk Tulia Ackson kwa kuaminiwa na kuweza kushika nafasi hiyo kubwa  Duniani.

Ndele amesema kuwa Chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Mbeya kitampokea Dk Tulia Ackson tarehe 11 Novemba 2023 akitokea jijini Dodoma na kwamba wanampongeza kwa namna ambavyo amekwenda kusimama na kuhiheshimisha ile azma na matamanio ya   Mwenyekiti wa Chama  cha Mapinduzi  Taifa na Rais Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwamba Spika wa mabunge Duniani atoke Tanzania.

Ndele Mwaselela amesema azma ya kufanya mapokezi hayo ni kumshukuru Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia  Suhulu Hassan kwa namna alivyo mpa ushirikiano mzuri DK Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Mbunge wetu anayetokana na Chama cha Mapinduzi ni fahari nafaja kwa wanambeya.

‘Ushindi wa DK Tulia kushika nafsi ya Urais katika Mabunge Dunia alama nzuri na ni historia nzuri kwa mkoa wa wetu wa Mbeya na huko duniani   sababu wataauliza anatoka wapi anatoka Mkoa wa Mbeya chama gani chama cha Mapinduzi  kwa hiyo ni furaha na faraja kubwa sana’ amesema Ndele MNEC kutoka  Mkoa wa Mbeya.

Katika hatua Nyingine Mnec Ndele amewataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya pasipo kuangalia itikadi za vyama kutokeza kwa wingi Novemba 11mwaka huu  katika viwanja vya shule ya Msingi Ruanda nzovwe kujitokeza na kushirika mapokezi hayo.