Thursday , 2nd Nov , 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo amesema Wafugaji Nchini hawana budi kuwa mabalozi wazuri na kuunga  mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi mazingira kwa kufanya shughuli za ufugaji wenye tija kwa maendeleo endelevu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo amesema ufugaji endelevu usioathiri hifadhi ya mazingira utasaidia  kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini.

“Tuepuke migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo tunashuhudia ikitokea katika baadhi ya mikoa nchini husababisha kutoelewana kwa makundi haya mawili hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani,”amesisitiza Waziri Jafo.