Wednesday , 1st Nov , 2023

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wakiongozwa na Andre Oanana wamelalamika kuwa jezi hasa za juu pamoja na soksi za klabu hiyo zinawabana na kuwanyima raha wanapokuwa michezoni.

Onana pamoja na Bruno Fernandes  ni miongoni mwa wachezaji waliolalamikia suala hilo, ambapo Onana kwa sasa havai tena jezi rasmi ambazo Adiddas wamewatengenezea na badala yake anavaa ambazo sio kwa ajili ya wachezaji (replica) ambazo hazimbani saana.

Wakati huo Bruno Fernandes nae havai soks rasmi, badala yake anavaa soks ambazo sio kwa ajili ya wachezaji, Adiddas watengenezaji wa jezi hizo wamesema wanafanyia kazi malalamiko hayo.