Neno FINTECH linaweza kuwa geni masikioni pako, lakini huwenda ukawa ni mmoja wa watu ambao umekwisha wahi kutumia teknolojia hii.
FINTECH ni kifupi cha neno ''Financial and Technology'' ukiweka kwa pamoja ndiyo unapata neno hilo, miamala yote iliyohitajika kukamilishwa mtandaoni, bila kusahau ile ya ku-tap na kuchanja ukijumlisha ile ya ku-scan basi yote inapita mbele kwenye hii.
Hizi ni baadhi tu ya faida za kutumia teknolojia hii ya FINTECH
1. Kurahisisha malipo yaani kupitia teknolojia ya FINTECH wewe ni sehemu yoyote tu una scan umamaliza au una-tap shughuli unaikamilisha.
2. Kubana matumizi kwani kupitia FINTECH huna hata ya kusubiri chenji ufanyapo malipo unaweka pesa inayotakiwa na inayobaki inasalia kikashani, yaani hapa haipotei hata hamsini.
3. Kukopa mtandaoni, iwapo muamala umeshindikana kukamilika kwa kukosa kiasi cha fulani cha fedha basi bank au taasisi husika ya kifedha inakuwezesha kukamilisha mualala kwa kukuwezesha (kukukopesha) kiasi kilichopelea.
4. Kufanya miamala ya fedha mtandaoni: ikiwa ni mtu wa kupenda ku-bet, kucheza games mtandaoni, kuagiza bidhaa mtandaoni na mengine yanayohusiana na hayo basi FINTECH ina nafasi yake kwenye hicho unachokifanya.
Picha: Saturadar.com