Monday , 30th Oct , 2023

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Duniani FIFA imemfungia Rais wa zamani wa shirikisho la soka nchini Uhispania Luis Rubiales kujihusisha ama kushiriki shughuli zote zinazohusiana na soka katika ngazi za kitaifa na kimataifa kwa kwa miaka mitatu (3).

Adhabu hii imetolewa kufuatia kitendo cha Rubiales kumbusu nyota wa timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania Jenni Hermoso, wakati timu ya taifa ya Uhispania walipoibuka washindi wa Kombe la Dunia la Wanawake, Kitendo ambacho kiliibua maswali mengi na kukashifiwa vikali duniani kote.