Monday , 30th Oct , 2023

Mwanamuziki Harmonize amefunguka nguvu kubwa aliyoiweka kwenye video mpya ya ngoma yake "Sijalewa" atakayoiachia Ijumaa hii akiwekeza pesa nyingi, muda mwingi na akili nyingi. 

Harmonize

Ameshare kipande kifupi cha Lyric video ya "Sijalewa" kupitia page yake ya Instagram na kuandika

"Nikumbushe ya kwamba hii mlioitazama mara Milioni 1.5 ni Audio. Video ya Sijalewa nimewekeza pesa nyingi, muda mwingi na akili nyingi".

Pia Harmonize ataachia Album yake mpya ya Visit Bongo na Nne tangu kuanza muziki siku ya Novemba 24.