Monday , 30th Oct , 2023

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba wanaotuhumiwa kumteka na  kumtishia kwa Silaha Honey Noah (29) mkazi wa Masaki jijini Dar es salaam

Inaelezwa kuwa  walimteka akiwa ndani ya gari lake aina ya Rav 4 na kumshikilia kwa nguvu kwa kipindi cha siku nne wakidai kiasi cha Dola milioni 3.5 kwa baba yake

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro anasema kutokana na chunguzi za kisayansi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao mmoja wapo ni raia wa Canada mwenye asili ya Kisomalia


Aidha Kamanda Murilo anasema watuhumiwa wote siku ya Leo watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili za  kumteka, kumtishia kwa silaha, kumshikilia kwa nguvu na kudai pesa kwa nguvu