Thursday , 19th Oct , 2023

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dokta Damas Ndumbaro amesema watatumia mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League 2023 kujiweka kwenye ramani nzuri kama nchi katika kuomba kuandaa mashindano mbalimbali kufanyika nchini Tanzania .

Waziri Ndumbaro amesema hayo kuelekea mchezo wa ufunguzi baina ya Simba dhidi ya Al Ahly ambapo utachezwa Ijumaa ya Oktoba 22-2023 huku mpaka sasa Marais 54 kutoka kwenye mashirikisho ya soka barani Afrika wakiwa tayari wamewasili hapa nchini kushuhudia mchezo huo.

“Mechi  sio ndogo, ukiangalia Simba ni timu ya saba inakutana  na timu iliyokuwa ya kwanza katika msimamo wa Afrika. Hii mechi kwa wachezaji wa Simba Sc  ni kipimo tosha kwa kuona ubora wao”amesema Ndumbaro

Lakini pia unaona jinsi gani mashindano haya yalivyombeba kila mtu kwa sababu msanii wa Tanzania Ally Kiba atakuwa sehemu ya kuwapa burudani ya muziki kwa wageni watakashuhudia mchezo huo," amesema  Ndumbaro.

Aliongeza kuwa  Tanzania imepata heshima nyingine kwa mchezo wa TP Mazembe dhidi ya Esperance itachezwa hapa nchini katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

.