Thursday , 19th Oct , 2023

Will Smith amepigia misumari msemo wa 'Funika kombe mwanaharamu apite' baada ya kufunguka kuwa Jada Pinkett ndio 'Bestfriend' wake bora kuwa naye duniani pia ataendelea naye kumsapoti kwenye maisha yake yote.

Picha ya Will Smith na Jada Pinkett Smith

Will Smith amefunguka maneno hayo ya upendo mbele ya Jada watoto wao Willow na Jaden Smith pande za Baltimore Marekani.

"Jada ni Best friend wangu bora kuwahi kuwa naye hapa duniani, nitaendelea kujitokeza kwa ajili yake na kumsapoti kwa maisha yangu yote" amesema Will Smith.

Jada Pinkett ametrend mitandaoni baada ya kufanya interview kadhaa Marekani kusema ametengena na Will Smith miaka 7 iliyopita, kuibua story za mahusiano yake na Tupac na issue za madawa ya kulevya.