Wednesday , 18th Oct , 2023

Nyota wawili Youcef Atal wa klabu ya Nice ya Ufaransa na Anwar El Ghazi wa klabu ya Mainz ya Uholanzi wamesimamishwa kazi na klabu zao mara baada ya kuweka ujumbe kwenye kurasa zao za mtandao wa Instagram ujumbe ambao unaiunga mkono Palestina.

Uongozi wa klabu ya Mainz ya Uholanzi umeeleza kuwa umemsimamisha kazi El Ghazi kwa sababu ujumbe/maoni yake hayaendani na maadili ya klabu. Huku Nice wao wamemsimamisha Youcef Atal mpaka pale taarifa zaidi itakapotolewa na klabu.