Tuesday , 17th Oct , 2023

Muigizaji wa filamu na Mtangazaji Jada Pinkett Smith amefunguka kuwa yeye na Will Smith wanapambania kurudisha ndoa yao licha ya kutengana kwa miaka saba.

Jada Pinkett Smith na Will Smith

Kupitia mahojiano aliyofanya na Hoba Kotb kuipitia Today Show Jada amesema "Mimi na Will tunapambana kwa bidii katika kuleta uhusiano wetu pamoja na ni kama tuko mahali ambapo tupo katika nafasi ya kina ya uponyaji wa uhusiano kati yetu".

Jada na Will walifunga ndoa mwaka 1997, walipata watoto wawili wakiwa pamoja ambao ni Jaden na Willow.