Monday , 16th Oct , 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekanusha ripoti za kusitisha mapigano ili kuruhusu "wageni" kutoka Gaza Kusini na "msaada wa kibinadamu kuingia"

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Misri inaweza kufungua tena njia ya Rafah kwa saa kadhaa   lakini kwa sasa imefungwa.

Maelfu ya watu wanakusanyika kwa matumaini ya kuondoka Gaza kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa kufanywa na Israel.

Wakati huo huo, jeshi la Israel linasema linahamisha jamii 28 ndani ya kilomita 2  kutoka mpaka wa Lebanon.

Pia imesasisha idadi ya Waisraeli ambao inaamini wanashikiliwa mateka huko Gaza - kutoka 155 hadi 199

Rais wa Marekani Joe Biden ameitaka Israel kuchukua tahadhari, wakati jeshi lake likijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini Gaza.

Zaidi ya watu 1,400 nchini Israel waliuawa katika mashambulizi ya Hamas wiki moja iliyopita; Watu 2,700 wameuawa katika mashambulizi ya Israel.

Karibu Wapalestina milioni moja sasa wanaaminika kukimbia kuelekea kusini kutoka kaskazini mwa Gaza - afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa amesema, kabla ya kile kinachotarajiwa kuwa mashambulizi makubwa ya ardhini na Israel.

Mpaka wa Rafah bado umefungwa licha ya umati wa watu kukusanyika kwenye milango na kuongezeka kwa miito ya chakula, vifaa vya matibabu na mafuta kuruhusiwa kuingia Gaza

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani Antony Blinken amewasili mjini Tel Aviv kwa ajili ya mikutano baada ya siku kadhaa za diplomasia, kusafiri kati ya mataifa ya Kiarabu.