Monday , 16th Oct , 2023

Mahakama nchini India imewaachia huru wanaume wawili ambao walihukumiwa kifo kwa miaka mingi kwa ubakaji na mauaji ya wanawake na watoto 19 mwaka 2005.

Surinder Koli na mwajiri wake mfanyabiashara Moninder Singh Pandher walipatikana na hatia mwaka 2009 katika kesi ya kutisha ambayo iliishtua nchi.

Walizuiliwa mwaka 2006 baada ya viungo vya mwili kupatikana karibu na nyumba yao karibu na Delhi.

Siku ya Jumatatu, Mahakama Kuu ya Allahabad ilimkuta Koli hana hatia katika kesi 12 ambapo alikuwa amehukumiwa kifo.

Mahakama pia imemkuta Pandher hana hatia katika kesi mbili dhidi yake. Wanaume hao wawili waliachiwa huru kutokana na "ukosefu wa ushahidi", wakili wao ameviambia vyombo vya habari. Hukumu kamili ya mahakama bado haijatolewa.

Mauaji hayo yalijitokeza mwaka 2006 baada ya viungo vya mwili na nguo za watoto kupatikana ndani ya maji taka mbele ya nyumba ya Moninder Singh Pandher katika kitongoji tajiri cha mji mkuu wa Noida.

Takriban wasichana 19 na watoto walibakwa, kuuawa na kukatwakatwa. Polisi walidai wakati huo kwamba mauaji hayo yalifanyika ndani ya nyumba ya Pandher, ambapo Koli alifanya kazi kama mtumishi.