Friday , 13th Oct , 2023

Nyota wa Newcastle United Sandro Tonali na mwenzake Nicolo Zaniolo wa Aston Villa wameondolewa kwenye kambi ya kikosi cha timu ya taifa ya Italia Azzuri kutokana na kupisha uchunguzi kutoka kwa waendesha mashtaka nchini Italia kuhusiana na vitendo vya ubashiri kwa wachezaji michezoni..

Taarifa ya chama cha soka nchini Italia FIGC imesema wachezaji hao hawana hali nzuri ya kushiriki kwenye michezo miwili   dhidi ya Malta na England kwa ajili ya kufuzu  michuano ya Ulaya 2024 nchini Ujerumani na hivyo wameruhusiwa kurejea kwenye klabu zao.

Mapema Alhamisi Oktoba 12-2023 Waendesha mashtaka wa FIGC walitangaza uchunguzi dhidi ya kiungo wa Juventus  Nicolo Fagioli kuhusu na ushiriki wake usivyo halali wa kubashiri mitandaoni huku Italia ambao ni bingwa mtetezi wa michuano ya Ulaya inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi C  wakiwa na  alama 7 mpaka sasa.