Friday , 13th Oct , 2023

Shirikisho la soka la Italia limewaondoa kambini wachezaji wake Sandro Tonali wa klabu ya Newcastle na Nicolò Zaniolo wa Aston Villa na kuwarudisha kwenye klabu zao kutokana na tuhuma za kucheza kamari kinyume cha sheria.

Wachezaji hao wanafanyiwa Uchunguzi ambao ni madai ya kamari ambayo hayajapitia kwa watengenezaji kamari wa kawaida wenye leseni, wakati huo huo kiungo wa kati wa Juventus Nicolo Fagioli nae anafanyiwa uchunguzi wa aina hiyo.

Endapo watakutwa na hatia, wachezaji hao wapo hatarini kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitatu.