
Baba aliyehukumiwa miaka 30 jela
Akisoma hukumu hiyo namba 114 ya mwaka 2023, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Manyoni Alisile Mwankejela, amesema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo usiku wa tarehe 03/07/2023 wakiwa nyumbani kwake huko kijiji cha Chibumagwa Kata ya Msakile.
Amesema kuwa siku ya tukio mshtakiwa alimwambia binti yake aingie ndani akalale na yeye kufunga mlango, kisha akaingia ndani kwa binti yake huyo mwenye umri wa miaka 14.
Baada ya kuingia chumbani binti akawasha tochi na akamuona baba yake kisha akaanza kufanya tendo hilo, ilipofika asubuhi ya tarehe 03/07/2023 binti akaanza kuhisi maumivu ndipo akaamua kwenda kwa jirani ambaye ni shahidi namba 3 kuelezea tukio hilo ndipo wakaenda ofisi ya mtadaji kutoa taarifa.
Mwankejela akiendelea kusoma hukumu hiyo amesema baada ya kufikishwa katika mahakama hiyo mshtakiwa alipotakiwa kutoa utetezi na kumuuuliza swali mhanga wa tukio hilo ambaye ni mtoto wake mshtakiwa alishindwa kuuliza swali lolote hali ambayo ilionesha wanafahamiana.
Huku mshtakiwa akisema kuwa mtoto wake alikuwa anaota kufanyiwa tendo hilo na amekuwa na uhasama nae kwa kile alichodai kutaka kwenda kuishi kwa ndugu upande wa mama yake jambo ambalo mahakama ililitupilia mbali kwa kukosa mashiko.