
Awali wazazi pamoja na wananchi waligoma kuzika mwili wa mwanafunzi huyo kufuatia kile kilichodaiwa kuwa mwanafunzi huyo alitumwa maji na mwalimu wa shule huyo kwa ajili ya matumizi yake huku wakiiomba serikali kugharamikia mazishi baada ya mwalimu kutoonyesha ushirikiano kwao
Aidha Kaka wa Marehemu Mwita Gibuka amethibitisha kuwa tayari familia hiyo imekaa pamoja na Uongozi wa shule hiyo na kusuluhisha tatizo na tayari wako tayari kuzika baada ya kusaidiwa kugharamikia mazishi ya Marehemu binti yao
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Makonge Kijiji cha Gibaso kilichopo kata ya Kwihancha Mwita Gasaya ambapo ndipo nyumbani kwao marehemu anaeleza kuwa mpaka Sasa hali ni tulivu na jamii imeshiriki kikamilifu katika mazishi hayo