
Wananchi wa Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga wamemlilia mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga ambaye ni Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdala dhidi ya mgogoro wao wa mpaka kati ya wilaya ya Kilindi na Kiteto mkoani Manyara uliodumu kwa muda mrefu sasa.
Wakizungumza mbele ya Mlezi wa chama hicho Hemed Suleiman Abdulla viongozi wa wilaya ya kilindi wanaomba kuharakishwa kwa mchakato wa mpaka huo ili kuepukana na migogogro kati ya wakulima na wafugaji .
"Mgogoro wa mpaka kati ya Kilindi na Kiteto mlezi wetu mgogoro huu tunasema ni mdogo kwasababu waziri Mkuu alishafika akatoa maelekezo wapimaji wamepita kilichobakia ni kusoma GN peke ake na kuweka mipaka ili kila mmoja ajue mpaka wake, "alisema
Mbunge wa jimbo la Kilindi Omari Kigua alisema jambo hilo limekuwa likileta usumbufu mkubwa hasa kwa viongozi wa serikali kwa kuwa wamekuwa hawasimamii miradi ya maendeleo kwajili ya migogoro ya kila siku kati ya wafugaji na wakulima.
"Suluhu ya kudumu ya jambo hili ni kuweka alama kubainisha eneo la mpaka kati ya kiteto na Kilindi kwa kuwa wote ni watanzania watu wa Kiteto wote ni Wanguu, wamasai na tulikuwa tukiishi kwa amani kwa muda mrefu hivyo tunaomba jambo hili lifanyiwe kazi kwa haraka, "alisema.
Katika majibu yake Mlezi wa Chama hicho Makamu wa pili wa Rais Zanzibar ameahidi kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa mpaka huo kumaliza mgogogro huo uliodumu kwa muda mrefu.
Makamu wa pili wa Rais amesema kuwa suala hilo la mpaka kati ya Kilindi na Kiteto inakwenda kumalizika kwa haraka iwezekanavyo kwa kuwa juhudi kubwa zinaendelea kuchukuliwa na serikali ili kumaliza tatizo hilo.
"Niwaombe sana wanakilindi tuendelee kuwa watulivu na kudumisha amani tukiamini serikali yetu ya chama cha mapinduzi inapenda sana wananchi wake waishi vizuri na jambo hili la migogoro watanzania wote hatulipendelei liendelee kubaki bila ya kupatiwa ufumbuzi kwakuwa athari yake tumeshaiyona siku hadi siku, "alisisitiza Makamu wa pili wa Rais.
Mgogogro huo umekuwa ukisababisha usumbufu kwa viongozi wa serikasli pale ambapo wanashindwa kusimamia miradi ya maendeleo wakijikita kwenye migogogro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikihatarisha maisha kati ya jamii hizo