Thursday , 12th Oct , 2023

Israel imesema kuwa kuzingirwa kwa Gaza hakutaisha hadi mateka wa Israel watakapoachiwa huru

 Waziri wa nishati Israel Katz anasema kuwa "Hakuna swichi ya umeme itakayowashwa, hakuna maji ya maji yatakayofunguliwa na hakuna lori la mafuta litaingia,"

Takriban mateka 150 walitekwa katika Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel mwishoni mwa wiki na kusababisha vifo vya watu 1,200.

Zaidi ya watu 1,300 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi, ambapo watu 338,000 wameyakimbia makaazi yao.

Siku ya Jumatano, kituo pekee cha umeme huko Gaza kiliishiwa na mafuta, ikimaanisha kuwa eneo hilo linategemea jenereta

Na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu inaonya jenereta za hospitali zinaweza kukosa mafuta leo.

Jeshi la Israel linasema mashambulizi yake ya anga yanalenga mtandao mkubwa wa mahandaki wa Hamas.

Zaidi ya familia 95 za mateka zimeambiwa jamaa zao wamepelekwa Gaza , huku zaidi ya maroketi 5,000 yamerushwa kutoka Gaza tangu Jumamosi  Israel yashambulia zaidi ya maeneo 2,600 Gaza

Waisraeli wasiopungua 1,200 wameuawa na wengine zaidi ya 3,000 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya mwishoni mwa wiki ya Hamas.