
Moshi ukifuka kufuatia shambulio la Israel katika ukanda wa Gaza
kutokana na kwamba wanao wapiganaji wengi
Hamad ameongeza kuwa tangu waanze mashambulizi walituma wapiganaji 1,200 ambao walifanikiwa kuuharibu uso wa Israel pamoja na usalama wake licha ya kwamba Israel kujulikana ni Taifa lenye nguvu.
Aidha kiongozi huyo ameongeza kuwa watu kutoka mipaka ya Jordan, Lebanon na kwingineko wako tayari kuwaunga mkono ili kuendeleza ghasia zake dhidi ya Israel.
Wakati hayo yakiendelea Waziri wa Nishati wa Israel amesema kuwa hakuna huduma za msingi ikiwa ni pamoja na umeme na mafuta ama misaada ya kibinaadamu itakayoruhusiwa kuingia Gaza hadi pale wanamgambo wa Hamas watakapowaachia Waisraeli waliowachukua kama mateka.