Wednesday , 11th Oct , 2023

Kikosi cha Simba SC Kinatarajia kuingia Kambini rasmi kesho Alhamis ya Oktoba 12,2013 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League dhidi ya Al Ahly ya Misri utaopigwa Oktoba 20 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally kuwa  Hii ndio michuano mikubwa zaidi barani Afrika na inashirikisha watu bora pekee na watu bora Tanzania ni Simba SC hivyo wamejipanga kupata ushindi katika mchezo.

"Hili sio jambo la kawaida na sio tu mchezo lakini ni ufunguzi wa michuano hi. Hili ni jambo kubwa zaidi kutokea kwenve historia ya mpira wa miguu Tanzania hivyo mashabiki wajitokeze kuja kushuhudia Simba SC anavyomfunga AL Ahly  “amesema Ahmedy.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Imani Kajula amesema  Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe atakuwepo na marais wa vyama va soka maeneo mengine akiwemo Rias wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino katika mechi ya uzinduzi wa 'African Football League' Simba dhidi Al Ahly Oktoba 20 mwaka huu.

Michuano hiyo ya Africa Football ligi inashirikisha timu nane kutoka katika nchi nane za Afrika zitakazo wania ubingwa wa AFL ambapomashindano hayo yatachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.