Tuesday , 10th Oct , 2023

Kamisheni ya ngumi za kulipwa Nchini (TPBRC) kupitia Kamati yake ya Nidhamu imetangaza kumfungia Bondia Hassan Mwakinyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kosa la kushindwa kupanda ulingoni kwenye pambano lililoandaliwa na kampuni ya uandaaji wa michezo ya PAF.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Katibu Mkuu wa TPBRC, George Lukindo amesema, mbali na adhabu hiyo Mwakinyo ameamriwa kulipa faini ya Shillingi Milioni 1 na adhabu hiyo inaanza leo Oktoba 10 mwaka 2023 na kumalizika Oktoba 10 mwaka 2024.

“Walikaa na kuzungumza na pande zote mbili na kubaini  kuwa vielelezo na maelezo ya  Mwakinyo hayakuwa na sababu zenye mashiko hivyo kulazimika kumuadhibu, Mwakinyo amepewa adhabu hiyo baada ya kuonekana kukiuka taratibu za mkataba wake dhidi ya Promota Godson Karigo,amesema  Silas.

Mwakinyo amepewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya kipindi cha siku 7 kuanzia siku ya kutangazwa hukumu hiyo.