Tuesday , 10th Oct , 2023

Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Chelsea na Real Madrid na timu ya Taifa ya Ubelgiji Eden Hazard ametangaza rasmi kustaafu kucheza mpira wa miguu akiwa na umri wa miaka 32.

Hazard anastaafu huku akiwa amecheza zaidi ya mechi 700 na kufanikiwa kufunga mabao 200 huku akiwa na idadi ya makombe 15.