![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/10/10/web.jpg?itok=8Y5GVBkZ×tamp=1696938523)
Simba SC ndio timu pekee iliyoshinda michezo yote mitano (5) ikiwa na wastani wa ushindi wa asilimia 100 (100%) na ndio vinara wa Ligi wakiwa na alama 15 kwenye michezi hiyo wamefunga mabao 14 na wamefungwa mabao 4.
Ni timu tatu ndio ambazo bado hazijashinda mchezo hata 1 katika michezo 5 iliyochezwa mpaka sasa. Timu hizo ni Coastal Union ya Tanga wamefungwa michezo 3 sare 2 wana alama 2 wapo nafasi ya 16, sawa na Mtibwa Sugar nao wana alama 2 wapo nafasi ya 15. Namungo FC nao hawajaonja radha ya ushindi wamefungwa michezo 2 sare 3 wana alama 3.
Yanga SC ndio timu iliyofunga mabao mengi, timu ya wanachi imefunga mabao 15, na wamefungwa goli 1 kwenye michezo yote 5 waliyocheza.
Yanga na Azam FC ndio timu zilizoshinda michezo mingi kwenye viwanja vya nyumbani, timu zote zimecheza michezo 3 na wameshinda michezo yote wamekusanya alama 9 kwenye viwanja vyao vya nyumbani.
Na Simba SC ndio timu iliyoshinda michezo mingi ugenini. Simba imeshinda michezo yote ya ugenini michezo 3. Katika alama zao 15 alama 9 wamezipata kwenye viwanja vya ugenini.
Ligi kuu itaendelea tena Oktoba 23,2023. Baada ya kumalizika kwa kalenda ya kimataifa ya FIFA na michezo inayofuata yay a raundi ya 6.