Swiatek mwenye umri wa miaka 22 amemshinda Mrusi Liudmila Samsonova baada ya kumfunga kwa seti 2-0 yaani 6-2 na 6-2 na kutwaa taji hilo la 5 baada ya kushinda mataji manne kabla ya French Open, Doha, Stuttgart na Warsaw ndani ya mwaka huu.
Iga Swiatek aliisimamisha rekodi ya ushindi wa mara 16 mfululizo kwa bingwa wa US Open 2023 Mmarekani Coco Gauff kwenye hatua ya nusu fainali huku sasa anashika nafasi ya pili kwa viwango vya ubora wa tenisi kwa upande wa wanawake duniani.