
Ilivyo ili upate nafasi ya kupata huduma za mtandao wa Netflix inakupasa kulipia kiwango fulani cha fedha, lakini ilikuwa tofauti na nchini Kenya ambapo kampuni hii ilileta huduma kwa lengo la kila mmoja kufurahia huduma zao nchini Kenya.
Taarifa mpya na ambayo inaweza kuwa mbaya kwa watumiaji wa huduma hii kutokea nchini Kenya, Ni kwamba kuanzia 1/11/2023 ndiyo itakuwa tamati ya kutumia huduma za bure kwenye mtandao huo, hivyo ili mtumiaji awezeshwe kupata huduma atahitajika kulipia kiwango cha fedha.