Tuesday , 3rd Oct , 2023

Michuano ya wazi ya tenisi ya Australia (Australia Open) kuanzia mwaka 2024 yatafanyika kwa siku 15 kwa ajili ya kupunguza michezo mingi kuchelewa kumalizika Usiku sana kwenye viwanja vya Melbourne Park nchini Australia.

Mkurugenzi wa shindano hilo Craig Tiley amesema tumezingatia ushauri wa wachezaji na mashabiki kupunguza suala hili na kuendelea kutoa fursa sawa kwa wachezaji kushindana ndani ya viwanja vya tenisi.

Hatua ya mabadiliko hayo yametokana na malalamiko ya mchezo baina ya Muingereza Andy Murray dhidi ya Muastralia Thanasi Kokkinakis ulioanza saa 22:20 Usiku na kumalizika 4:05 Usiku na kufanya mchezo huo kutumia masaa 5 na dakika 45 kwenye michuano ya mwaka huu  huku michuano ijayo ya Australia Open inataraji kuanza kufanyika kuanzia  Januari 14-2024..