Wednesday , 27th Sep , 2023

Kwenye mahojiano yake na Mathias Döpfner ambaye ni mkurugenzi mkuu wa makampuni ya ''Axel Springer SE'' Bilionea namba moja Duniani Elon Musk amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kudai kwamba kwa mtazamo wake anadhani kuwa Vladimir Putin ambaye ni Rais wa urusi ni tajiri zaidi yake.

 

Mathias : Kuwa na utajiri zaidi ya Dola Bilion 230 unatajwa kuwa tajiri namba moja Duniani

Elon Musk : Nadhani Putin anautajiri mkubwa zaidi yangu, 

Mathias : Unaamini hivyo?

Elon Musk : Sawa, Ninachojaribu kumaanisha siwezi kuvamia nchi na vilivyomo, Nina amini kwenye msemo wa zamani wa Crassus unaosema "Bado huwaja tajiri mpaka uwe na uwezo wa kumiliki jeshi" 

Huyu Marcus Crassus ni moja kati ya viongozi wa Romani aliyehesabiwa kuwa na utajiri mkubwa kwa wakati huo, aliwahi kusema utahesabiwa kuwa tajiri pale tu ambapo kipato chako kitaweza kumiliki jeshi.