Friday , 15th Sep , 2023

Uongozi wa klabu ya Azam Fc umesema malengo yao makubwa kwa sasa ndani ya msimu huu wa mwaka 2023-24 ni kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara na Kombe la shirikisho la Azam Sport Federation.

Akitoa tambo hizo Mkurugenzi Habari na Mawasiliano, Azam FC Thabit Zakaria maarufu 'Zaka za Kazi' amefurahi kuona katika mechi mbili walizocheza katika uwanja wao nyumbani wa Azam Complex Chamazi wamepata matokeo mazuri hivyo amepata imani kubwa.

''“Tunawatumia Salamu Klabu zote ambazo zitakuja kucheza Chamazi katika uwanja wetu lazim waache alama tatu kwani tumedhamiria kutokana na muunganyiko wa kikosi chetu kwa sasa”amesema Thabit Zakaria

Kwa upande mwingine:'Zaka za Kazi' amewataka mashabiki na wapenzi wa Azam FC kuwa wa moja katika kipindi hiki licha ya wao kutolewa katika mikwaju ya Penati 4- 3 katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi Bahir Dar ya Ethiopia.