
Wananchi hao wanadai kwamba mradi wa maji wa zaidi ya shilingi milioni 290 ulielekezwa katika kijiji chao lakini ghafla walishangaa mradi huo umehamishwa bila taarifa na sasa wanaletewa maji ambayo ni ya chumvi ilhali tathmini ya awali ilionesha chanzo cha maji kitatoka katika kata yao na chanzo hicho wanaamini kina maji mazuri zaidi.
Aidha wanasema mgomo huo umechangiwa pia na suala la Fedha ambapo wanadai mradi huo ulitoweka ghafla na hawakujua fedha za mradi huo zimekwenda wapi na kipi kimefanyika.
Wakijibu suala hilo Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wamedai mradi huo waliuhamisha baada ya kuona kuwa maji kijijini hapo hayatoshi
"Tulimwagiza mtaalamu afange vipimo kabla ya ujenzi wa mradi, tukagundua chanzo cha Lionja kina mabadiliko na hakiwezi kukidhi haja ya wananchi wote... ndio tukahamisha na kupeleka Namikango" amesema Timotheo Abel ambaye ni afisa kutoka RUWASA
Naye mbunge wa jimbo la Nachingwea ambaye alishiriki katika kikao hicho na wananchi, amelaumu kuwepo kwa changamoto ya ushirikishwaji, katika kikao hicho na wananchi yeye pamoja na uongozi wa Wilaya, wamewaomba wananchi kukubali kutumia maji hayo kwani fedha nyingi tayari zimetumika katika mradi huo