
Akizungumza na vijana waliopatiwa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa mujibu wa sheria operesheni miaka 60 ya jeshi la kujenga Taifa katika kikosi 838 Maramba JKT kilichopo Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi Brigedia General Fabian Gasper Machemba amewasisitiza vijana hao kuyatumia vyema mafunzo hayo.
Aidha aliwataka vijana hao kuheshimu na kuzingatia maamuzi yao na kufuata yale yote waliyofundishwa kuyatumia vizuri katika jamii inayowazunguka.
"Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmelitendea haki wemyewe lakini mmelitendea haki jeshi la kijenga taifa na jamii mlipotoka na Taifa kwa ujumla, "alisistiza Brigedia
Awali akifunga mafuzo hayo Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanal Maulid Surumbu amewataka vijana waliohitimu mafunzo hayo kutumia taaluma waliyopatiwa kambini hapo kuwa msingi wa kujiajiri wenyewe kwa manufaa yao na Taifa ujumla.
"Ni matumaini yangu kuwa taaluma na ujuzi mliopata kupitia mafunzo haya itakuwa ni msingi wa kujiajiri wenyewe huko muendako na kwa manufaa yenu lakini pia kwa Taifa kwa ujumla lakini pia mtambue kwamba Taifa lina matarajio makubwa sana kwenu na ndio maana tumetumia gharama kubwa sana kuwaweka hapa kwa majuma 12 na leo mmeiva kweli kweli, "alisema Kanal Surumbu.
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha 838 Maramba JKT Ashraf Hassan amesema kuwa vijana hao wamefundishwa masomo mbalimbali kwa nadharia na vitendo ikiwemo utimamu wa mwili na uzalendo.
"Vijana hawa wamefundishwa mmasomo mbalimbali kwa nadharia na vitendo ikiwemo uzalendo kwa nchi yao na uzalishajo mali, "alibainisha.
Baadhi ya wahitimu waliomaliza mafunzo hayo wameiomba serikali iwaongezee muda wa kuendelea kupatiwa mafunzo hayo yanayowajengea uzalendo wa nchi yao huku wakitoa shukrani kwa serikali.