Wednesday , 6th Sep , 2023

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi amesema nchi hiyo inapaswa kupunguza kasi ya kuzaa ili kuepuka janga. 

Rais huyo amesema Misri inapaswa kupunguza watoto wanaozaliwa kwa mwaka hadi 400,000 kutoka zaidi ya milioni mbili ya sasa ili nchi hiyo iweze kutoa ajira na huduma za kijamii kwa ufanisi kwa raia wake

Hivi karibuni Waziri wa afya wa nchi hiyo Bw Khaled Abdel Ghaffar alisema kuzaa watoto ni suala la uhuru kamili jambo ambalo limekosolewa na Rais huyo

"Lazima tupange uhuru huu la sivyo utaleta janga," amesema Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi 

Alidokeza kuwa Misri inaweza kuiga sera ya China ya mtoto mmoja, kwani China huku akisema China ilifanikiwa katika sera yao ya kudhibiti idadi ya watu

Tangu mwaka wa 2000, idadi ya watu nchini Misri imeongezeka kwa milioni 40 hadi kufikia watu milioni 105