
Akizungumza na EATV Mwalimu mkuu wa shule hiyo Juliana Kusigwa wakati wa mahafal ya 51 ya shule hiyo ambayo imefanyika katika ukumbi wa GEDECO uliopo mjini Geita amesema uchakavu wa majengo hayo unatokana na majengo hayo kukaa muda mrefu bila kukarabatiwa nakuwaomba wadau wa elimu mkoani hapa jitokeza kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu inchini.
“Wadau mbalimbali wanaotusikiliza shule yetu inaitaji watu wajitolee kufanya maboresho,serikali wanajitahidi sana lakini bado kuna mapungufu kama hayo,swala la maktaba kweli tuna uhaba sana hatuna chumba cha maktaba lakini hata vile vitendea kazi vya ndani ya maktaba hatuna,pia tuna ukosefu wa chumba cha darasa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu hakuna miundombinu rafiki kwakweli”
Aidha kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema changamoto kubwa zinazowakabili ni ukosefu wa maktaba pamoja na ubovu wa jiko la kupikia chakula.
“Shule yetu tunakabiliwa na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa jiko la kupikia maana mvua inapo nyesha maji uingia ndani kwaiyo chakula akiwezi kupikika kwa urahisi kutokana na maji kuingia”
“Maktaba yetu ina upungufu wa vitabu ili mwanafunzi kuongeza ufanisi katika masomo yake lakini pia ubovu wa jiko la kupikia maana mvua inaponyesha jiko linaloana wapishi wanakosa pakIpiki”
Mgeni rasmi katika mahafari hiyo Jumanne Yusufu Mtafuni ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya dhahabu amepokea ombi la kuwa mlezi wa shule hiyo na kuahidi kushirikiana na serikali katika kuboresha mazingira ya shule hiyo.
Mimi ni mzaliwa wa hapa Geita nimeamua niwe mlezi wa hii shule ili kuwashawishi wadau wengine kushirikiana na serikali ili tusonge mbele watoto wetu wa wakisoma wakafaulu tunajivunia maana hawa ndo viongozi wa baadae “
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule Bw.Emmanueli Kalwanizi akaitimisha kwa kutoa shukrani kwa mgeni rasimi kuridhia kuwa mlezi wa shule hiyo huku akitoa wito kwa wadau wa elimu mkoani hapa kuungana kwa pamoja kuisaidia shule hiyo