
Wakizungumza baada ya Baraza la Waislam BAKWATA ambao wameshirikiana na wadau wengine kuwajengea Zahanati, wamesema licha ya jitihada zao wanazozifanya lakini bado wanaomba huduma ya maji ipatikane kwa haraka ili yawasaidie majumbani, shuleni na kwenye kituo hicho cha Afya.
Changamoto ya maji kwao imekuwa kero kwani wanalazimika kusafiri umbali mrefu ili kupata maji safi huku baadhi ya akina mama wakiwa ni wazee wasio na uwezo wa kutembea kitambo kirefu na wenye ukata wa fedha kwani hawawezi kuabiria bodaboda kuwatekea maji.
"Inafkia hatua mtu haogi hadi siku mbili kwasababu hakuna maji, ili upate maji lazima uende mbali au ukodi bodaboda.... ni maporini watu wanakutana na simba na wengine wanakufa kwa kudhuriwa na wanyama" alisema Hawa Shaibu, mkazi wa Ruyaya.
Aidha, kukosekana kwa maji kunaonekana kuteteresha ndoa za akinamama wa kijiji cha hicho, ambacho wanaume wamekuwa wakali na mara kadhaa wamekuwa wakiwapiga wake zao kwasababu ya kuchelewa kurudi nyumbani wakiwahisi huenda walikuwa kwa wanaume wengine.
"Tunatoka usiku tunakwenda Namanolo - ni huko Porini alafu kuna Simba na milima mikubwa, tunakwenda na tunalala huko huko, tunapigwa na wanaume zetu kwasababu wanaona tunachelewa" Asha Selemani
Kuhusu suala la Afya wakazi wa Ruyaya walikuwa wanatembea umbali mrefu kuifwata Zahanati, kwa jitihada zao kwa kushirikiana na BARAZA KUU LA WAISLAMU TANZANIA BAKWATA, wameweza kupata Zahanati Mpya.
Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir ndiye aliyeizindua Zahanati hiyo, katika kusikiliza kero za wananchi ameahidi kuyawasilisha hayo katika sehemu husika huku akipongeza jitihada za ujenzi wa Zahanati na kuwataka Waislamu wote nchini kubadilika na kufanya mambo ya maendeleo hasa kutatua kero za wananchi.