Thursday , 31st Aug , 2023

Mtoto Mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Msowero Kilosa mkoani Morogoro, amechomwa na maji ya moto kwenye makalio pamoja na kuchapwa viboko mgongoni na mjomba wake pamoja na shangazi yake  aliyekuwa akiishi naye kisha kutokomea kusikojulikana huku chanzo cha tukio hakijajulikana.

Kutokana na tukio hilo la kikatili kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilosa ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Shaka Hamdu Shaka, kumtembelea  mtoto huyo  aliyelazwa katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Dumila ili kuona anavyoendelea.

"Namuagiza Mkurugenzi kuhakikisha mtendaji wa Kata pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii wa Kata husika wanakamatwa kwa kutoshughulikia hali ya mtoto wakati walipata taarifa na naagiza pia kukamatwa kwa shangazi na mjomba wa mtoto popote walipo," amesema DC Shaka.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi hospitali ya Mtakatifu Joseph Dkt Selemani Sakoro, na msamaria aliyejitolea kumsaidia mtoto huyo Bi Caroline Makemo nao wakaeleza hali aliyokuwa nayo mtoto huyo.

Na hapa Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima, amelaani vikali juu ya tukio hilo la ukatili kwa mtoto huo.