
Miili mingi iliyoungua moto mjini Johannesburg inaweza kuwa vigumu kuitambua kwa kuwa imeteketezwa zaidi ya kutambuliwa
Jengo la ghorofa tano katikati ya jiji hilo haijulikani ni nini kilichosababisha moto huo.
Maafisa wanasema wazima moto waliwahamisha wakazi wa jengo hilo walipowasili, na shughuli ya kutafuta na kurejesha miili inaendelea.Ripoti zinasema kuwa wengi wao walikuwa wahamiaji kutoka Afrika
Miongoni mwa waliouawa ni watoto saba, akiwemo mtoto mchanga wa miezi 18, msemaji wa idara ya huduma za dharura mjini Johannesburg Robert Mulaudzi amesema. Watu 52 wanatibiwa kutokana na majeraha.
Imeelezewa kuwa hilo ni moja ya matukio mabaya zaidi ya moto mjini Johannesburg katika historia ya hivi karibuni na kuna hofu kwamba idadi ya vifo itaendelea kuongezeka wakati wafanyakazi wa uokozi wakiingia katika ghorofa zilizobaki za jengo hilo la ghorofa tano.
Miili mingi iliyoungua moto mjini Johannesburg inaweza kuwa vigumu kuitambua kwa kuwa imeteketezwa zaidi ya kutambuliwa, ripoti ya kituo cha televisheni cha Newzroom Afrika imesema.