Monday , 28th Aug , 2023

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemkamata Ibrahim Elisha (55) mkazi wa Ngara, Kagera na Nyokindi Anatory (44) mkazi wa nchi jirani (Burundi) kwa tuhuma za wizi wa pikipiki tatu zenye thamani ya shilingi Milioni 11.8, mali ya halmashauri ya wilaya ya Sengerema idara ya Afya. 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Willbroad Mutafungwa, akionesha pikipiki hizo

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Willbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea tarehe 20, Agosti 2023 katika kituo cha afya Mwabaluhi, wilayani Sengerema ambapo wahalifu hao walivunja ofisi ya mganga mkuu wa wilaya hiyo na kuiba pikipiki hizo tatu kisha kwenda kuziuza nchini Burundi.

Watuhumiwa wamehojiwa kwa kina na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani