Tuesday , 24th Feb , 2015

Star wa muziki wa R&B mwenye makazi yake huko Australia, Rama Dee ametoa mtazamo wake katika muda mfupi aliokuwa hapa nchini kuwa, amefurahi kuona kuwa kwa sasa katika sehemu mbalimbali za burudani, muziki wa kiafrika unapewa nafasi zaidi.

Rama Dee

Rama Dee amesema kuwa, changamoto pekee aliyoiona ni kushikiliwa kwa soko na muziki wa Nigeria zaidi, akiamini kuwa Bado pia muziki wa hapa nyumbani wanaweza kufanya kitu cha ziada na kushindana na muziki unaofanya Nigeria na sehemu nyingine.