Wednesday , 16th Aug , 2023

Uongozi wa klabu ya Singinda Fountan Gate FC, umeweka wazi kuwa malengo yao katika michuano ya kimataifa ni kuhakikisha inafika katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Singida inatarajiwa kushuka dimbani ijumaa ya Agosti 18,2023 katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya JKU ya Zanzibar katika uwanja wa Chamazi Complex majira ya saa moja usiku

Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa. habafi  wa Singida Fountain Gate FC Hussen Massanza amesema  timu yao imejipanga vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano hayo na kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa kutinga katika hatua ya makundi.

“Sisi ndo tunashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo, lakini tunamikakati mizuri kuhakikisha tunatimiza malengo tuliojiwekea ya kufikia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika,” amesema  Massanza.

Naye mtendaji mkuu wa Singida Fountan Gate FC, Sikwane Olebile amesema  ameingia katika timu hiyo kuhakikisha anaenda  kuboresha ili iweze kuwa bora zaidi ya ilivyokuwa zamani.

amesema  anajua msimu uliopita wamemaliza nafasi ya nne hivyo anahitaji msimu huu timu yao ifike katika nafasi ya juu zaidi.

“Tumemaliza nafasi ya nne msimu uliopita na malengo makubwa ambayo nahitaji msimu huu ni kufika nafasi ya juu zaidi,” amesema  Olebile.