Tuesday , 23rd Jan , 2018

Uongozi wa Hospitali ya Mawenzi iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro, umetoa maelezo juu ya malalamiko yaliyotolewa na wananchi kwenye kipindi cha SupaMix kinachorushwa na East Africa Radio, ambayo yanawapelekea kupata ugumu wa matibabu.

Malalamiko hayo ambayo yameelezwa kwamba wananchi wanaokwenda kupata huduma kwenye hospitali hiyo ambayo ni ya serikali, hawapatiwi matibabu mpaka ukate 'Tembo Card' yenye gharama ya elfu 10, 400, na ndipo uweze kupatiwa matibabu, na iwapo ukirudi mara ya pili ndani ya wiki utalazimika kulipia elfu 3, na ikiwa utarudi baada ya mwezi mmoja, utalazimika kulipia elfu 8 ndipo uanze kutibiwa, achilia mbali gharama za vipimo na dawa.

Akijibu tuhuma hizo Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo Richard Kafwila ametoa maelezo ambayo yanaonekana ya kusuasua, juu ya gharama za malipo ya kadi hiyo.

Sikiliza hapa chini jinsi alivyokuwa akijibu suala hilo