Monday , 14th Aug , 2023

Timu ya Taifa ya kriketi Tanzania imeingia rasmi kambini kujiandaa na mashindano ya kuwania kufuzu kushiriki kombe la dunia ambayo yatarajiwa kuanza Novemba 20,2023 mwaka huu nchini Namibia

Mkurugenzi mtendaji chama cha kriketi Tanzania  Hamis Abdallah amesema kuwa wameanzaa matayarisho ya timu yao  mapema  kwa kupata mechi za kirafiki nchini Rwanda hivyo watakwenda na wachezaji  14 .

"Tumeingia Kambini mapema kwaajili ya kuanza mazoezi na tunatambua ni mashindano makubwa ambayo kwa Afrika zinatakiwa zitoke timu mbili "amesema Hamis Abdallah Mkurugenzi Mtendaji Kriketi.

Wakati huo huo Nahodha wa timu hiyo Mohamed Yunusi amesema  kuwa wameanza mazoezi mapema ya kujiandaa na mashindano huku akitoa pongezi kwa uongozi wake katika ukuaji wa mchezo huo hapa nchini.

Mashindano hayo ya kuwania kufuzu kushiriki kombe la dunia kwa upande wa Kriketi yatashirikisha nchini zaidia ya nane kutoka katika ukanda wa Afrika .