
Bwana Bazoum, mwenye umri wa miaka 63, anashikiliwa mateka na mkewe na mwanawe na kulikuwa na wasiwasi kuhusu afya zao.
Hii ni ishara ya hivi karibuni kwamba serikali ya junta inatarajia kupinga shinikizo la kimataifa la kurejesha madaraka kwa Bw Bazoum.Amekuwa akizuiliwa katika ngome ya ikulu yake tangu jeshi lilipofanya mapinduzi wiki tatu zilizopita.
Bwana Bazoum alikuwa katika roho nzuri licha ya kushikiliwa katika hali ngumu, daktari wake alisema baada ya ziara.
Ziara hiyo ya Jumamosi iliidhinishwa huku kukiwa na ongezeko la mahitaji ya kimataifa ya kutaka Bw Bazoum aachiliwe huru.
Lakini katika ishara kwamba inaimarisha msimamo wake, serikali ya kijeshi imesema katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa kwamba imekusanya ushahidi wa kumshitaki rais aliyeondolewa madarakani na washirika wake wa ndani na nje kwa uhaini wa hali ya juu na kudhoofisha usalama wa ndani na nje wa Niger.
Msemaji wa serikali ya Junta Hakutoa maelezo zaidi.
Bwana Bazoum, mwenye umri wa miaka 63, anashikiliwa mateka na mkewe na mwanawe na kulikuwa na wasiwasi kuhusu afya zao.
Jenerali Abdourahmane Tchiani, mkuu wa kitengo cha walinzi wa rais, alijitangaza kuwa mtawala mpya wa Niger tarehe 26 Julai baada ya kumpindua.
Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi Ecowas imetishia kuchukua hatua za kijeshi za kuyapindua mapinduzi hayo, lakini hadi sasa imeshindwa kutekeleza kitisho chake.Viongozi wa mapinduzi wameonya kuwa watajilinda dhidi ya uingiliaji wowote.
Ecowas pia imeiwekea vikwazo serikali ya nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kupunguza umeme nchini Niger. Hali hii imesababisha kukatika kwa mji mkuu Niamey na miji mingine mikubwa.
Siku ya Jumamosi, ujumbe wa viongozi wa dini ya Kiislamu kutoka nchi jirani ya Nigeria ulikutana na viongozi wa junta mjini Niamey katika juhudi za kutafuta suluhu ya mgogoro huo.