Saturday , 12th Aug , 2023

Mkutano uliotakiwa kuwakutanisha Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra umeakhirishwa kwa muda usiojulikana kulingana na tamko lilitolewa jana Ijumaa na vyanzo vya kijeshi kwenye jumuiya hiyo.

Vyanzo hivyo vilisema mkutano huo ulikuwa umeandaliwa ili kuwaeleza viongozi wa ECOWAS juu ya "njia bora zaidi" za kuunda na kutuma kikosi hicho cha dharura nchini  Niger. 

Bado ECOWAS haijafafanuwa undani wa kikosi hicho wala ratiba ya hatua zake, huku viongozi wake wakisisitiza kuwa bado wanataka suluhisho la amani.