Thursday , 10th Aug , 2023

Viongozi wa Afrika Magharibi wanakutana Alhamisi hii kujaribu kuamua iwapo watatumia nguvu za kijeshi au diplomasia kurejesha demokrasia nchini Niger.

 

Ni wiki mbili tangu Rais wa Niger alipokamatwa na walinzi wake ambao wakati huo walitwaa madaraka, ikiwa ni mara ya hivi karibuni katika msururu wa mapinduzi ya kijeshi yanayoenea kote barani humo.

Viongozi wa jumuiya ya Ecowas wanakutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja. Mkutano huo unatajwa kuwa haitakua rahisi sana. Viongozi hao Wana hamu ya kurejesha demokrasia nchini Niger , taifa kubwa, maskini ambalo tayari linapambana na waasi wa Kiislamu.

Wakati huo huo Kiongozi wa junta nchini Niger Jenerali Abdourahmane Tchiani ameteua baraza la mawaziri kinyume na wito wa viongozi wa kikanda wa kumrejesha madarakani rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

Baraza la mawaziri lilitangazwa kwenye televisheni ya serikali leo. Serikali mpya inaundwa na mawaziri 21, wakiwemo mawaziri wawili wa nchi na waziri wa mjumbe.

Serikali mpya ya mpito, inayoundwa na wanajeshi na raia, inaongozwa na Waziri Mkuu wa mpito Lamine Zeine Ali Mahamane, ambaye pia ataibuka mara mbili kama waziri wa uchumi na fedha.

Tayari serikali hiyo imewateua wakuu wapya wa jeshi na kuwafuta kazi maafisa wengi wa ngazi za juu wa serikali ambao walihudumu katika utawala wa Bw Bazoum.