Monday , 24th Jul , 2023

Jeshi la polisi Jijini Mwanza linamshikilia Osward Kaijage(39) dereva na mfanyakazi wa mgodi wa GGM Geita, ambaye alisababisha vifo vya watu sita na kujeruhi wengine 16 katika ajali iliyotokea Jumamosi eneo la Sabasaba Ilemela wakati watu hao wakifanya mazoezi.

Gari lililogonga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amesema dereva huyo amekamatwa eneo la Kisesa na bado anahojiwa na jeshi hilo na pindi upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Aidha Kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa vikundi vyote vinavyofanya mazoezi ya mchakamchaka kujisajili kwenye ofisi za utamaduni katika ngazi ya wilaya, manispaa na jiji ili wapate miongozi au maelekezo ya namna bora ya kufanya mazoezi kwa kuzingatia hali ya usalama wao na watu wengine

Katika hatua nyingine viongozi wa vikundi hivyo vya mazoezi watakutanishwa katika uwanja wa Nyamanaga siku ya Jumamosi kwa ajili ya kupewa elimu ya usalama barabarani na mambo muhimu wanayotakiwa kuzingatia wawapo barabarani wakati wa michezo ili kuepusha ajali.