Friday , 21st Jul , 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi balozi wa nchi yake nchini Uingereza.Vadym Prystaiko hivi karibuni alikosoa majibu ya rais huyo kwa mzozo juu ya shukrani kwa msaada wa kijeshi wa Uingereza.

Balozi Vadym Prystaiko amekua balozi wa Ukraine nchini Uingereza tangu mwaka 2020

 

Balozi huyo alikuwa ameita ahadi ya Bwana Zelensky ya kumshukuru waziri wa ulinzi wa Uingereza kila asubuhi  kejeli zisizo  na afya. Kyiv haikutoa sababu rasmi ya kufukuzwa kazi lakini ilithibitisha kuwa Prystaiko hakuwa balozi tena.

Mapema mwezi huu, Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema ameionya Ukraine kwamba   inahitaji kuonyesha shukrani kwa silaha ilizopokea ili kuwashawishi wanasiasa wa Magharibi kutoa zaidi.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa Nato baada ya Rais Zelensky kukosoa muungano wa kijeshi kwa kuchelewa kuifanya Ukraine kuwa mwanachama.Matamshi ya Wallace yalichochea hasira mjini Kyiv na baadaye alisema maneno yake yalikuwa  yametafsiriwa wa vibaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alijibu kwa kusema anajiuliza ni  kiasi gani Ukraine inathamini msaada wa Uingereza.

Balozi Vadym Prystaiko alikuwa katika wadhifa wake mjini London tangu mwaka 2020 lakini siku ya leo Rais Zelensky alitoa amri ya rais kutangaza kufutwa kazi kwake, akisema pia ameondolewa kama mwakilishi wa Ukraine katika Shirika la Kimataifa la Bahari.